Wachezaji wa Yanga walio fanya vizuri na vibaya jana
Wachezaji Yanga walio fanya vizuri na vibaya jana.
1. Youthe Rostandi: huyu jamaa kwa siku ya jana hakua kwenye kiwango kabisa ni mungu tu ndio katuokoa kuna mipira kama miwili aliyo itema pale golini kwake Rayon wangekua makini wange jipatia goli.
2. Hasani Kessy: kacheza kwa kiwango cha juu sana jana licha ya kwamba tatizo lake la hasira halijawahi kumuacha salama jana kacheza vizuri sana ila apunguze hasira.
3. Gadiel Michael: huyu nae alicheza vizuri sana hakua na tatizo lolote kwenye upande wake ameitendea vzr haki nafasi yake.
4. Endwro Chikupe: Nimoja ya mabeki bora kabisa kwa sasa wanao patikana hapa nchini jana alidhihirisha hilo alikua mhimili mkubwa wa safu ya ulinzi yanga kifupi alicheza vizuri kabisa.
5. Kelvin Yondani: Nahodha huyu amendelea kuonyesha umuhim wake kwenye kikosi cha yanga jana alifanya kazi kubwa ya kuwazuia Rayon uwepo wake jana uli saidia kwa kiasi kikubwa sana.
6. Thaban Kamusoko: Alicheza vizuri sana kwa dakika zote alizo kuepo uwanjani alitengeneza mashambulizi na kutuliza vizuri timu sehemu ya kiungo hakukua na sababu ya kutolewa labda benchi la ufundi wanajua sana kuliko sisi.
7. Juma Mahadhi: unaweza kusema huyu ndio nyota wa mchezo kwa siku ya jana mahadhi alikua ana peleka mshambulizi mbele pasi zake zote zilifika kwa wenzake kwenye safu ya ushambuliaji yanga mahadhi pekee ndio alikua mtu hatari kwa Rayon.
8. Pius Buswita. Huyu sijajua kwanini alimaliza dk 90 alipoteza mipira mingi sana katikati ya uwanja alishindwa kabisa kuwalisha mipira washambuliaji wake kiufupi hakucheza vzr jana.
9. Obrey Chirwa. 😂 Huyu jamaa siku hizi sijui nini kimemkuta licha ya kwamba mipira mingi alikua hapelekewi mbele lakini hata ile michache iliyo mkuta hakuitendea haki kama tunavyo mjua labda mchezo wa jana ulimkataa mapema.
10. Yusuphu Mhilu: Hakucheza vizuri sana wala hakucheza vibaya sana alijitahidi kadri ya uwezo wake lakini alishindwa kutamba kama tunavyo mjua.
11. Godfrey Mwashiuya: Bado ana mambo ya kitoto ali poteza mipira mingi kizembe kabisa.
Makala By Dozeeh Brand
0 komentar:
Post a Comment